Breaking News: Basi la Ally's na Isanzu Coaster Yagongana Uso Kwa Uso

Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya Isanzu si nzuri. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi. Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga. Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Mfaume amesema amepokea majeruhi 35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

No comments