JUKWAA LA KATIBA LAIPINGA BAJETI YA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI bunge la kupitisha Bajeti ya mwaka 2017-2018 likianza vikao vyake leo mjinia Dodoma ,huku bajati hiyo ikiwa ukomo wake kufikia trioni 31.6 kutoka trioni 22 za mwaka wa fedha unaoishia mwezi juni mwaka huu, Jukwaa la katiba nchini (JUKATA) limeibuka na kuonyesha masikitiko kwa serikali kwa kushindwa kutekeleza bajeti ya trioni 22 inaoyoishia mwaka huu na badala yake serikali imekuja na bajeti kubwa ambapo wameshindwa kutekeleza bajeti ndogo iliyopita.. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa Mtendaji wa (JUKATA) Hebron Mwakagenda amesema wamebaini utekelezaji duni wa bajeti ya mwaka 2016 -2017 hasa kwenye miradi ya maendeleo . ‘Tumeona bajeti hii inayoishia serikali ilipanga kutumia trioni 29.5 katika mwaka 2016-2017 ,fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya mwaka unaoelekea mwisho serikali ilitenga trioni 11.8 (40%) ya bajeti kuu,JUKATA tumesikitishwa na taarifa za serikali kwamba hadi mwezi wa tatu serikali imepeleka trioni 3.5 (34%) ya miradi ya maendeleo ,’amesema Mwakagenda. Mwakagenda amesema itakuwa ajabu kama serikali itaendelea kuleta bajeti ya trioni 30.1 2017-2018 ya mwaka huu ambayo amedai haitekelezeki

No comments