CHOZI LA MOYO (Sehemu Ya NNE)

Na Janeth Frank Tulipo ishia Anna ameamua kumsikiliza babaake na kukubali kweda Dar es salaam kusoma chuo sasa Endelea nayo ujue nini kitaendelea baada ya apo …. Baada ya mwezi ya mmoja Anna alilazimika kujiandaa kuondoka Iringa kwa mama ake mdogo nakuja Dar es salaam kwa Babaake alifurahi sana kwakuwa alikuwa anajua atakutana na mpenzi wake Tobby, Anna alimwambia mpenzi wake Tobby kuwa anakuja dar kusoma . Tobby alifurahi sana nakumsii Anna amsikilize na kumuheshimu Babaake . Zikapita siku tatu Anaa kawa amesha wasili Dar es salaam pia alimueleza mpenzi wake kuwa amekuja Dar es salaam kwa Babaake anaeishi Mabibo lakini pia Tobby nae anaishimaeneo ya Temeke_Mikoroshini.(kwale wale wakazi wa Dar es salaam wanazifahamu sana sehemu hizi ni uswahilini lakini ni baadhi ya sehemu sio zote) Maisha yaliendelea Anna na Tobby yaliendelea japo hawakupata muda wakuonana kwakuwa kila mtu alikuwa bize na shughur za hapa na pale. Ilipofika mwezi wa kumi Anna alianza kusoma computer katika chuo kimoja apo jijini Dar es salaam kwa kozi ya miezi mitatu kwaajili ya mafunzo ya computer,Wakati huo Tobby alikuwa field hatimae akamaliza na kupata kazi ya kusambaza Filamu za BONGO yeye akiwa kama Graphic Disner. Tobby akamueleza Anna kwenye simu kuwa amemaliza mafunzo na amepata kazi Anna alifurahi sana kusikia habari izo na kumpongeza Tobby na kumwambia Nakupnd sana mpenzi wangu Mungu atusaidie sana tufikie malengo yetu ,Tobby akajibu nakusema Mungu yupamoja nasi ana na wew soma kwa bidii,Sikuiyo Tobby na Anna walifurahi sana . Sikumoja Tobby alikuwa anatoka Mwenge akampigia simu Anna nakumuuliza yuko wapi anaomba kuonananae maeneo ya UBUNGO kama hatojali kwakuwa alikuwa amemkumbuka sana na anaitaji kumuona,Anna akatoka kwao Mabibo na kwenda mpaka Ubungo kwania ya kukutana na mpenzi wake Tobby alipofika Anna alimpigia simu Tobby kakumuuliza yupo Ubungo maeneo gani maan yeye alikuwa amesimama OIL COM(pembeni kidogo ya Ubungo stand) Tobby alimwambia Anna simama apoapo ,Kumbuka Anna ni mgeni na jiji la Dar es salaam ivyo hakuwa akizijua sehemu za mitaa vizuri alisimama palepale kuendelea kumsubili mpenzi wake Tobby. Baada ya kugeuka tuu Anna hakuamini machoyake kwa alichokiona….Itaendelea usikose sehemu ya TANO ya hadithi nzuri ya CHOZI LA MOYO…Je,Anna aliona kitu gani na nini kilitokea baada ya hapo.

No comments